Klabu
ya soka ya Arsenal imefika robo fainali ya Kombe la FA baada ya kuilaza Sutton
United kupitia mabao ya Lucas Perez na Theo Walcott.
Katika
mechi hiyo iliyochezewa Gander Green Lane, Wenger alifanya mabadiliko saba katika
kikosi kilichochapwa 5-1 na Bayern Munich mechi ya mkondo wa kwanza hatua ya 16
bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wiki iliyopita.
Kikosi
chake kilikuwa an nguvu za kutosha kuwazidi wapinzani hao ambao wamo nafasi 105
chini yao katika orodha ya ustadi wa klabu Uingereza.
Lucas
Perez alifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 26 naye Theo Walcott akaongeza
la pili dakika 10 baada ya kipindi cha pili kuanza.
Ushindi
huo ulimpunguzia shinikizo meneja Arsene Wenger na Arsenal sasa watakutana na
Lincoln City katika robo fainali ukizingatia Lincoln walifika robo fainali kwa
kuwalaza Burnley Jumamosi.
Mchezo
mwingine unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ni ule kati ya
Chelsea na Man U ambao wanatarajia kukutana robo fainali FA.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.