Hatimaye watanzania Haruna Chanongo na Abuu Ubwa
wamefanikiwa kufuzu majaribio yao baaada ya kwenda katika klabu ya TP Mazembe
ya DR Congo kufanya majaribio hao na wanasubili sasa kusaini mikataba tu na
klabu hiyo.
Meneja wa wachezaji hao, Fadhili Mtemi au Mataifa ambaye pia anafanya kazi na Jamali Kasongo ameiambia Kilowoko.blogspot.com kwa njia ya simu kuwa mambo yote yamekwenda vizuri na kinachosubiriwa ni Mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi, kutoa maamuzi ya mwisho juu ya wachezaji hao wawili kuichezea timu hiyo kuanzia msimu ujao.
Mtemi alikiri na kuesema wao walipokea taarifa hizo kwa njia ya mdomo lakini kikubwa wanachokisubiri kwa sasa ni taarifa kwa njia ya maandishi ambayo itachukua takribani wiki moja kujua kinachoendelea juu ya wachezaji hao.
“Kwa hivi sasa tunasubiri taarifa rasmi ya maandishi kutoka katika uongozi wa klabu hiyo kutokana kuwa tumepata taarifa za mdomo tuu ambayo huwezi jua,” Alisema Mataifa.
Na hawa wanakuwa wachezaji wengine wa 4 kama wakichukuliwa na klabu ya Mazembe ambayo imejenga imani na wachezaji wa Kitanzania baada ya kuridhishwa na wachezaji wawili wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Na huenda Thomas Ulimwengu sasa machungu yakamuisha kutokana na watanzania hao kuchukuliwa baada ya ndugu yake Samatta kupata ulaji nje .
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.