Klabu ya soka ya Simba hii leo imeenza vizuri ligi
baaada ya kupata pointi 3 muhimu ilipokutana na wapinzani wao klabu ya soka ya
Mtibwa Sager mchezo ulioigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dae es
Salaam.
Mshambuliaji Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliipa klabu Simba
SC matumaini ya kushinda baada ya kufunga bao safi katika dakika ya 5 ya
mchezo akimalizia mpira uliopigwa na Ibrahim Hajib kutoka upande wa kushoto.
Simba SC sasa inafikisha pointi 30 baada ya kucheza
mechi 14, ikiendelea kukaa nafasi ya tatu nyuma ya Yanga SC yenye pointi 32 ikisubili
mchezo wake wakesho dhidi ya Ndanda huku vinara, Azam FC ikiwa na pointi 35 ikisubiri
mchezo wake wa baadae hii leo.
Mtibwa Sugar walionyesha upinzani kwa Simba SC na
dakika ya 11, kiungo Shiza Kichuya alipoteza nafasi ya wazi baada ya shuti lake
kuokolewa na kipa Vincent Angban, raia wa Ivory Coast.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.