Na Nicolaus Kilowoko.
Christopher Maurice "Chris" Brown ni Mwanamuziki,mnenguaji lakini pia ni muandishi wa nyimbo aliyezaliwa mnamo mwezi Mei, mwaka 1989 katika mji wa Tappahannock, Virginia, nchini Marekani.
Christopher Maurice "Chris" Brown ni Mwanamuziki,mnenguaji lakini pia ni muandishi wa nyimbo aliyezaliwa mnamo mwezi Mei, mwaka 1989 katika mji wa Tappahannock, Virginia, nchini Marekani.
Chris Brown alifanikiwa kuwa ni miongoni mwa vijana
ambao alianzia kipaji chake cha kuimba katika kwaya kanisani akiwa na umri
mdogo zaidi.
Na alifanikiwa kusaini katika lebo ya “Jive Records”
mwaka 2004, na mwaka mmoja baadaye aliweza kutoa albamu yake ya kwanza.
Brown alichaguliwa kuwa mwanamuziki katika nafasi ya
pili kwa ubora duniani kutokana na mauzo ya kazi zake ambapo alifanikiwa kuuza
kopi ya nakala za nyimbo zake zaidi ya Sh. Milioni tatu.
Katika nyimbo yake moja aliyoipachika jina la "Run
It!" alifanikiwa kuuza zaidi na kufanikiwa kuwa mwanamuziki wa kwanza wa
kiume kuuza zaidi tangu mwanamuziki mwenzake Diddy afanye hivyo mwaka 1997.
Brown katika albamu yake ya mwaka 2007 iliyobeba
nyimbo kama "With You" na "Forever" ilikuwa ni albamu bora
zaidi kuuzwa duniani na kumuwezesha kupata fedha nyingi zaidi na kuweza kupata
mafanikio zaidi na kujulikana zaidi.
Mbali na kuimba mwenyewe lakini Brown kutokana na
kuanza kufanikiwa na kujulikana aliweza kushirikishwa katika nyimbo mbalimbali
ambazo alifanya vizuri zaidi na kuendelea kumletea umaarufu duniani.
Brown alishirikishwa katika nyimbo ikiwemo ile nyimbo
aliyoshirikishwa ya "No Air", na mwanamuziki Jordin Sparks,
"Shortie like Mine" aliyoshirikishwa na mwana muziki rapa Bow Wow na
"Shawty Get Loose" aliyoshirikishwa na Lil Mama na T-Pain.
Na nyimbo zote hizo zilifanikiwa kushika katika nafasi
kubwa katika orodha ya za ubora wa nyimbo duniani.
Kuna mambo kadhaa ambayo huyafahamu kuhusu Chris Brown
na yanaendelea kumuweka katika orodha ya wanamuziki mahiri miaka yote
ulimwenguni na kufanya muziki wake uendelee kupendwa ni pamoja na.
Brown ni kati ya wasanii wa kiume wanaopendwa zaidi
duniani na kufanya muziki wake kuwa ni kivutio kikubwa zaidi ulimwenguni na
amezidi kuwa mwanamuziki ambaye anazidi kuongeza ubora wake katika miondoko ya R&B
toka aanze kujulikana zaidi mwaka 2005.
Mbali na kufanya kazi yake ya uimbaji lakini pia Brown
ni muigizaji na alifanikiwa kuonekakana katika runinga katika tasnia hiyo mwaka
2007 ambapo alitokea katika filamu ya “This Christmas”, “Takers” mwaka 2010, “Think
Like a Man” mwaka 2012, na ya “Battle of the Year” mwaka 2013.
Brown amefanikiwa kushinda tuzo nyingi ulimwenguni na
akifanikiwa kushinda tuzo kumi na nne za “BET”, tuzo tano za “Billboard Music”
tuzo tatu za “Soul Train Music” na kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo mbalimbali inasemekana Brown ni kati ya wanamuziki mia
yeye ni wa saba duniani ambaye hajawai kuchuja na anaendelea kufanya vyema kila
leo.
Majabu mengine ya Chris Brown ni kuwa huwa mara nyingi
wanamuona shujaha na wanamfananisha na mwanamuziki mkongwe ambaye alifariki
miaka michache iliyopita “Michael Jackson” kutokana na kuweza kunengua vyema
akiwa jukwaani.
Maajabu mengine ni mbali na kuwa na umri wa miaka 25
lakini sauti yake huwa haishuki na wala haipandi miaka yote toka aanze kazi
yake ya muziki kwa maana ya kwamba ipo katika mstari ule ule wa kuimbia muziki.
Mbali na uimbaji lakini pia Brown ni mchezaji mzuri
sana wa mchezo wa mpira wa kikapu na lianza kucheza mchezo huo akiwa na umri wa
miaka sita aliweza kucheza timu ya wakubwa ambayo inawachezaji wenye umri wa kuanzia
miaka nane.
Wengi wetu tunafahamu na ni destuli pia kuwa mahusiano
ya mapenzi kwa watoto si jambo zuri kwani linaweza kuwafanya wasiweze kufika
katika malengo yao lakini Brown aliweza kutoa bikra yake akiwa na umri mdogo
zaidi wa miaka nane na ni jambo ambalo linamuumiza hadi leo.
Mbali na umaridadi wake katika muziki lakini pia Brown
amekuwa mwanamuziki ambaye hakosi vituko katika kazi yake ya muziki na kumfanya
kila leo aongelewe katika mitandao ya kijamii.
Mbali na vituko vyake lakini pia Brown ameingia katika
orodha ya wasanii wenye michoro mingi zaidi mwilini na kumfanya abadirike
katika kila kazi yake ambayo anaitoa kwa mashabiki wake na kumfanya awe tofauti
zaidi.
Kutokana na umahiri wake na kuweza kudumu katika
muziki wa ushindani mpaka sasa ingekuwa kwa kibongo Brown tunaweza kumfananisha
kama bando lisilo chacha na ukisikiliza nyimbo zake huwezi kuzipimia na
kuchagua nyimbo za kusikiliza.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.