
Timu ya soka ya vijana ya Tanzania umri chini ya
miaka 17 Serengeti Boys imeendelea na mazoezi yake hii leo katika uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ya
vijana na ya Congo ya kusaka nafasi ya kushiriki Fainali za vijana
zitakazofanyika nchini Madagasca mwaka 2017.
Mwenyekiti wa maendeleo ya soka la Viajana Kutoka
TFF Ayoub Nyenzi amesema baada ya kucheza mchezo wao dhidi ya timu ya Afrika ya
kusini na kuitoa katika kinyang’anyiro hicho sasa timu hiyo inatarajiwa
kuingiia kambi nchini Shelisheli ili kujiweka sawa zaidi na mchezo huo.
Mchezo huo wa Serengeti Boys dhidi ya Coongo
unatarajiwa kupigwa Septemba 18 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.