Waendesha mashtaka nchini Brazil wamependekeza
kwamba nyota wa timu ya Barcelona Neymar ashtakiwe na mashtaka matatu ya
ufisadi kuhusu kesi ya kodi wakati wa uhamisho wake hadi Barcelona.
Inadaiwa kwamba kampuni zilibuniwa ili kutumika kwa
niaba yake ili mchezaji huyo alipe kodi ya kiwango cha chini.
Maafisa nchini Brazil wanasema kuwa madai hayo dhidi
ya mshambuliaji huyo wa Barcelona yanasimamia kipindi cha miaka saba kuanzia
2006.
Madai hayo ni tofauti na yale ya kesi iliosikizwa siku
ya Jumanne nchini Uhispania.
Neymar alihudhuria kesi yake ya madai ya ufisadi
kuhusu uhamisho wake na Amekana kufanya makosa yoyote.
Madai hayo ya viongozi wa mashtaka yatakwenda kwa
jaji ambaye ataamua iwapo kuna kesi ya kujibu au la na kwa sasa Neymar sio
mshtakiwa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.