Patrice Latyr Evra ni raia wa nchini
Ufaransa aliyezaliwa mnamo miaka ya 1981ambaye kwa sasa anakipiga kunako katika
klabu ya Marseille.
Evra kiuhalisia kabisa katika mchezo
wa soka anacheza nafasi ya beki wa kushoto na kumfanya hadi aliyekuwa kocha
wake wa zamani Sir Alex Ferguson kumkabidhi mikoba ya Unahodha wa Manchester
United huku pia katika timu yake ya Taifa ya Ufaransa.
Evra asili yake kabisa alizaliwa
nchini Senegal na alielekea barani Ulaya akiwa na umri wa mwaka mmoja.
Alianza kujulikana katika ramani ya
soka hasa laipokuwa akikipiga katika klabu za CO Les Ulis na CSF Brétigny na
mnamo mwaka 1997, alianza rasmi kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Paris
Saint-Germain.
Mwaka mmoja baadaye Evra alianza
kujulikana na kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa zaidi katika nchi ya
Italia alipokwenda kusaini mkataba wa kuichezea klabu ya Marsala katika mji wa Sicily.
Evra Alizidi kuonyesha kiwango bora zaidi
na klabu yake hiyo kabla ya baadaye kujiunga na klabu ya Monza katika msimu
mmoja baadaye alirudi tena nchini nchini Ufaransa ambako alijiunga na klabu ya Nice.
Mwaka 2002, Evra aliekea kunako
katika klabu ya AS Monaco na kuiwezesha klabu yake kutwaa taji la ligi hiyo ya Coupe
de la Ligue mnamo mwaka 2003.
Alizidi kujiimarisha zaidi katika
mashindano mbalimbali na katika mwaka wake wa kwanza katika kazi yake ya mpira
katika msimu wa mwaka 2003–04 aliweza kucheza vyema katika nafasi yake ya beki
wa kushoto katika klabu yake ya Monaco na mwaka 2004 waliweza kushiriki katika
fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Na katika mwaka huo huo Evra aliweza
kukujumuishwa katika kikosi cha soka cha dunia na kuweza kutwaa tuzo ya
mchezaji bora kijana zaidi wa mwaka 2004.
Mafanikio ya Evra.
Mwaka 2006, Evra aliweza kujitanua
zaidi na kuweza kuelekea nchini Uingereza na kuweza kujiunga na klabu ya Manchester
United wakati huo klabu hiyo ikiwa nchini ya Alex Ferguson ambaye alithibitisha
usajili wake.
Evra alijiunga na klabu hiyo kwa
uhamisho huru ambapo alisaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa ada ya
uhamisho wa £5.5 million kabla ya misimu miwili kuanza kutolewa macho na klabu
nyingine za ulaya ikiwemo Arsenal, Liverpool na Real Madrid.
Klabu hizo zilianza mazungumzo na
wakala wake huku mwenyewe akiweka wazi kukataa kujiunga na klabu zingine zaidi
ya Manchester United ambayo alikuwa anaihusudu sana.
Evra ataja aliyemgomea kurudi United.
Baada ya kuondoka kunako katika
klabu ya soka ya Manchester United na kujiunga na klabu ya soka ya Juventus
Evra aliendelea kuwa na mapenzi na klabu ya Man U.
Evra alifunguka kuwa wakati akiwa
anataka kuondoka katika klabu ya soka ya Juventus ya Italia alitaka kurudi
katika klabu yake ya zamani ya Manchester United.
Wakati akiwa katika harakati za
kurudi United Evra alisema kuwa alijarbu kuongea na kocha wa sasa wa United
Jose Mourinho lakini alishangaa kugomewa na kucho huyo kurudi klabuni hapo.
Evra alisema kuwa alikuwa karibu
kutua tena Manchester United lakini alishangaa kocha huyo kumzuia kujongea
klabuni hapo na kufunga matumaini yake ndani ya viunga vya Old Trafford.
Evra alisema kuwa baada ya kuona Man
U inachelewa kumchukua akaamua kutangaza ofa kwa klabu nyingine ambapo klabu ya
Marseille iliweza kuchangamkia ofa hiyo.
Mlinzi huyo wa kushoto alihamia
Marseille hivi karibuni akitokea Juventus katika uhamisho wa dirisha la usajili
wa Januari mwaka huu.
Evra alisema kuwa kabla hajaondoka
katika klabu ya Juventus aliongea kwanza na kocha Mourinho kuhusu sula la
kurejea United lakini alimgomea kurudi tena katika klabu hiyo ya United.
Evra alisema kuwa baada ya kuona
hivyo alitangaza ofa ya kuelekea katika klabu yoyote ile na alishanga kuona
klabu ya Marseille kujitokeza haraka na kumtaka kujiunga na klabu hiyo.
Evra, kwa sasa ana umri wa miaka 35
na aliweza kudumu katika klabu ya United kutoka mwaka 2006 hadi 2014, alipoondoka
klabuni hapo na ameshinda mataji matano ya ligi kuu soka nchini Uningereza huku
akishinda tuzo kumi katika maisha yake ya soka mpaka sasa.
Mataji aliyowahi kubeba evra katika maisha yake ya soka
mpaka sasa.
Premier League (5): 2006–07,
2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
Football League Cup (3): 2005–06,
2008–09, 2009–10
FA Community Shield (5): 2007, 2008,
2010, 2011, 2013-14
UEFA Champions League (1): 2007–08
FIFA Club World Cup (1): 2008
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.