
TIMU ya taifa ya wanawake ya Nigeria wameandamana
nje ya bunge jijini Abuja wakidai bakshishi zao ambazo hazijalipwa.
Wachezaji hao waliandamana bungeni hapo wakati rais
Muhammadu Buhari akiwasili bungeni kwa ajili ya kuwasilisha bajeti yake katika
kipindi cha mwaka ujao.
Mabingwa wa Afrika baadae waliandamana tena mpaka
katika makazi ya rais Buhari ambapo mmoja wa wasaidizi wake alitoka na
kuwaambia wachezaji hao kuwa watalipwa katika kipindi kisichozidi siku mbili.
Wachezaji wamegoma kutoka katika hoteli waliyofikia
toka walipotoka katika michuano hiyo, mpaka hapo watakapolipwa bakshishi zao ambazo
ni dola 17,500 kila mmoja.
Taarifa kutoka jijini Abuja zimedai kuwa baada ya
maelezo hayo waliyopata kutoka kwa msaidizi wa Rais Buhari, wachezaji walirejea
hotelini kusubiri serikali itemize ahadi yake.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.