Manchester United usiku wa kuamka
hii leo mambo yalikuwa mazito na kunusuru alama moja wakicheza dhidi ya CSKA
Moscow katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Bao la Martial dakika ya 65
liliwawewezesha miamba hiyo ya Uingereza kuondoka nchini Urusi kwa ushindi
mwembamba wa sare ya bao 1-1 kwenye mechi hiyo.
Seydou Doumbia alikuwa amewapa CSKA
uongozi dakika ya 15, akiwa wa kwanza kufikia mpira baada ya kipa wa United
David de Gea kutema penalti iliyochapwa na Roman Eremenko baada ya Martial
kunawa mpira eneo la hatari.
Red Devils hao sasa wamo nambari
mbili Kundi B baada ya Wolfsburg kuilaza PSV Eindhoven na kutua kileleni.
Wapinzani wao wa Jumapili Manchester
City walifunga bao la dakika za mwisho na kuandikisha ushindi wa 2-1 dhidi ya
Sevilla katika mechi yao Ligi ya Klabu Bingwa iliyochezwa pia Jumatano usiku.
Matokeo mengine ya mechi zote za
Uefa zilizochezwa Jana ni:
Paris St Germain 0 - 0 Real Madrid
CSKA Moscow 1 - 1 Manchester Utd
Manchester City 2 - 1 Sevilla
Malmö FF 1 - 0 Shaktar Donetsk
VfL Wolfsburg 2 - 0 PSV
Atletico Madrid 4 - 0 FC Astana
Galatasaray 2 - 1 Benfica
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.