Mshambuliaji wa Manchester United,
Wayne Rooney amefaulu vipimo vya afya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya
Everton siku ya leo.
Nahodha huyo wa United alizikosa
mechi za kufuzu michuano ya Euro 2016 dhidi ya Estonia na Lithuania kutokana na
majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata katika mchezo waliotandikwa mabao 3-0 na
Arsenal kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Hata hivyo, sasa United
imethibitisha nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 yuko fiti na atakuwepo katika
mchezo huo dhidi ya Everton masaa machache kuanzia sasa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.