Katika taarifa yake shirikisho hilo lilisema kuwa shutuma zilizotolewa na gazeti la Der Spiegel hazikuwa na msingi wowote.
Gazeti hilo ambalo halikusema lilitoa wapi habari hizo lilisema kuwa karibu dola milioni sita zilitumika kununua kura kutoka kwa baadhi ya wanachama wa kamati kuu ya FIFA ili Ujerumani ipewe nafasi ya kuandaa kombe hilo.
FIFA inasema kuwa madai hayo dhidi ya Ujerumani yanatiliwa maanani na yatakuwa sehemu ya uchunguzi wa ufisadi katika mchezo wa kandanda duniani
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.