Klabu ya soka ya Real Madrid ya nchini Hispania
imeshindwa rufani yake ya kupinga kuenguliwa katika michuano ya Kombe la Mfalme
kwa kuchezesha mchezaji asiyeruhusiwa.
Mabingwa hao mara 19 wa michuano hiyo walienguliwa
kwa kumchezesha winga Denis Cheryshev katika mchezo dhidi ya Cadiz uliochezwa
Desemba 2 mwaka huu.
Cheryshev alipaswa kutumikia adhabu yake kutocheza
mechi moja ambayo aliipata wakati akicheza kwa mkopo Villarreal msimu uliopita.
Mahakama ya Michezo ya Hispania ilitupilia rufani ya
Madrid baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote kuhusiana na sakata hilo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.