Na Merina Robert
Morogoro
MABONDIA Francis Cheka bingwa wa ngumi za kulipwa dunia wa
uzito wa kati(WBF) na mwenzake Thomas Mashali kila mmoja ametamba kumpiga
mwenzake katika pambano lisilo na ubingwa linalotarajia kufanyika siku ya
sikukuu ya Kristimas Desemba 25 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wakizungumza mara baada ya kupima uzito mabondia hao
katika kituo cha mabasi Msamvu ambapo mabondia wote walikutwa na uzito wa
kilo 77 bondia Francis Cheka amesema amejiandaa vizuri na kwamba hawezi
kuzungumza zaidi anasubiri ulingoni huku bondia Thomas Mashali akisema kuwa
naye amejiandaa vizuri hivyo haogopi kupambana na bondia mwenye jina.
Kwa upande wake mmoja wa mabondia wanawake anayetarajia
kucheza kwenye pambano la Utangulizi Lulu Kayage na bondia mwenzake
wa kike Mwanne Haji amesema kuwa mabondia wanawake wamekuwa wakisahauliwa na
mapromota katika mapambano mbalimbali licha ya kuwa na uwezo mkubwa kwenye
mchezo huo na kuahidi kufanya vizuri kwenye pambano lake.
Naye mwandaaji wa pambano hilo Siraji Kaike amesema pambano
hilo litakuwa na ushindani mkubwa kutokana na mabondia wote kujiandaa vya
kutosha na kwamba matokeo yoyote yanaweza kutokea .
Katika pambano hilo litatanguliwa na
mapambano ya utangulizi baina ya mabondia Deo Njiku na Vicent
Mbilinyi,lulu Kayage na Mwanne Haji,Seba Temba na Pius Kazaura,Twaha
Kiduku na Ibrahim Clasic,Mohamed Matumla na Kudra Tamimu,Epson John na Sadick
Momba na Mfaume Mfaume na Kasim Mohamed.
Post a Comment