
Na Omary Katanga.
Dar es Salaam.
Michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam kwa msimu wa
mwaka 2015/2016 inaanza kutimua vumbi desemba 21,kwa michezo
minne kupigwa katika viwanja tofauti.
Timu ya Sifapolitan wataikaribisha timu ya Ninja,
Katika uwanja wa S/msingi kigamboni,timu ya Inter Milan watacheza dhidi ya timu
ya Red Coast katika uwanja wa M/nyamala,timu ya Kijitonyama watakipiga dhidi ya
Azania Ngano kwenye uwanja wa Kunduchi,huku timu ya Mkunguni wakioneshana ubabe
dhidi ya timu ya Magereza kwenye uwanja wa Magereza.
Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam inashirikisha jumla
ya timu 32 zilizopangwa a katika makundi manne, ambapo kila kundi linaundwa na
timu 9,zitakazomenya kusaka washindi watatu kila kundi watakaoingia kucheza
hatua ya pili,na washindi watatu wa jumla watakaopatikana,majina yao
yatapelekwa Tff kwaajili ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa.
Kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Dar es
salaam DRFA,imethibitisha kukamilika kwa maandalizi yote ya ligi hiyo,ikiwa ni
pamoja na kuzipa kanuni na taratibu klabu zote zinazoshiriki.
DRFA ina imani kuwa kama ilivyokuwa katika misimu
iliyopita,mashindano hayo yataleta ushindani wa kweli na hatimaye kuwajenga
kiuwezo wachezaji watakaojihakikishia kupata nafasi katika vilabu
vinavyoshiriki ligi daraja la kwanza na ligi kuu hapo baadaye.
Post a Comment