Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umeitaka klabu ya
soka ya Etoile Due Sahel ya nchini Tunisia kuhakikisha wanailipa klabu hiyo
mapema fedha za aliyekuwa mchezaji wao Emmanuel Okwi kabla ya kufikia mwezi March mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa klabu
hiyo Haji Manara amesema klabu hiyo ya Etoile Due Sahel iliandika barua kwenda
Shirikisho la soka Dunia FIFA kutaka kuongezewa muda wa kulipa deni lao ndani
ya klabu ya Simba Mwezi March mwakani jamabo ambalo uongozi wa Simba umepinga
suala hilo.
Klabu ya Simba inaidai klabu ya Etoile Du Sahel
takrimbani sh. milioni 600 kwaajili ya mchezaji wao Emmanuel Okwi ambazo
hazijalipwa hadi sasa nadani ya klabu hiyo.
Okwi alinunuliwa na Etoile Januari mwaka 2013 kwa
dau la dola 300,000sawa sawa na shilingi Milioni 600 za kitanzania ingawa baada
ya muda akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo ya Tunisia.
Mtafaruku ulianza baada ya Okwi kuchelewa kurejea
mjini Sousse mkoani Sahel baada ya ruhusa ya kwenda kuichezea timu yake ya
taifa, Uganda.
Okwi naye akadai Etoile walikuwa hawamlipi mishahara
na kufungua kesi FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa), ambayo mwisho wa siku
alishinda kwa kuruhusiwa kutafuta timu nyingine ya kuchezea kulinda kipaji
chake, wakati wa mgogoro wake na klabu ya Tunisia.
Hata hivyo, Okwi
mapema Oktoba mwaka huu, Simba SC nayo ilimuuza katika klabu ya SonderjyskE
FC inayoshiriki ya Ligi Kuu ya Denmark ambako amesaini Mkataba wa miaka mitano.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.