Klabu ya Arsenal usiku usiku wa kuamkia hii leo
imewatandika Manchester City mabao 2-1katika ligi kuu soka nchini Uingereza iliyoendela
usiku wa jana.
Wakiwa katika dimba la nyumbani Emirates Stadium
klabu ya Arsenal ilitawala saehemu kubwa ya mchezo huo hadi Theo Walcott na
Olivier Giroud walipotupia kila mmoja bao moja.
Man City ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia
kwa kiungo wake Yaya Toure aliyepata bao katika dakika ya 82 ya mchezo lakini
Arsenal wakaendelea kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.
Pamoja na ushindi huo wa jana lakini Arsenal
inaendelea kubaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 36 nyumba ya Leicester
City yenye pointi 38 katika msimamo wa Ligi Kuu Engaland.
Post a Comment