Baada ya kurindimba kwa ligi kuu soka Tanzania bara
jumamosi iliyopita sasa ligi hiyo kuendelea tena Desemba 26 mwaka huu kwa
michezo 6 kuchezwa katika viwanja tofati tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa habari wa
Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF Baraka Kizuguto amesema ligi hiyo
itaendelea tena jumamosi ijayo na siku ya jumapili ya Desemba 27 kwa michezo
miwili.
Kizuguto amesema pamoja na kuendelea kwa ligi kuu
lakini vile vile ligi daraja la kwanza itaendelea tena kwa mzunguko wa pili
Desemba 26 kwa michezo 10 kupigwa katika viwanja tofauti tofauti.
Katika hatua nyingine Kizuguto amesema baada ya
kuchezwa kwa michezo hiyo ya ligi kuu na ligi daraja la kwanza lakini kombe la
Shirikisho nalo litaendlea ili kumpata bigwa atakaye iwakilisha Tanzania katika
michuano ya Afrika Mwaka 2017.
Baada ya kufaika kwa michezo hiyo Desemba 26 ligi
itasimama kwa muda kupisha kombe la Mapinduzi hadi January 16 mwakani itakapoanza
tena kutimua vumbi lake.
Post a Comment