Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema
Mshambuliaji wake Alexis Sanchez atakuwa nje hadi mwezi Januari baada kupata
majeraha mapya.
Sanchez alipata majeraha ya mguu mwezi Novemba na
alitarajiwa kucheza katika mechi ya Ligi ambayo Arsenal walishinda mabao 2-1
dhidi ya Manchester City, sasa atakuwa nje kwa kipindi chote cha sikukuu ya
Krismasi.
Sanchez atarejea Januari 10 jambo ambalo linamlazimu
kuzikosa mechi dhidi ya Southampton, Bournemouth, Newcastle na Sunderland.
Lakini kocha wa klabu hiyo amesema walikuwa na
mpango wa kumwanzishia benchi dhidi ya Man City lakini alipata maumivu kidogo
wakati wa mazoezi siku mbili zilizopita.
Post a Comment