Baada ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili sasa
kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji inatarajiwa kuketi siku ya kesho
kwaajili ya kupitia mapingamizi ya wachezaji walio na matatizo katika usajili wao.
Afisa habari wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF
Baraka Kizuguto amesema kamati hiyo itaketi ikiwa na lengo la kupitia
mapingamizi yote ambayo wachezaji wwke walikuw na matatizo wakati wa
kusajiliwa.
Kizuguto amesema kamati hiyo itaketi katika viunga
vya karume jijini Dar es Salaam ili kuahakikisha wanapata muafaka kwa wachezaji
walio na matatizo ya klabu zao kwa ujumla.
Post a Comment