Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

CECH ANAIMANI MWAKA HUU NI WA ARSENAL KUTWAA UBINGWA WA EPL.



Cech: Arsenal will win Premier League 

Mlinda mlango wa klabu ya soka ya Arsenal Peter Cech amesema klabu yake inaweza ika twaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza kwa sababu ya kurejea kwa wachezaji wake wengi waliokuwa katika majeraha.


Cech amesema baada ya kurejea kwa wachezaji wengi wa klabu hiyo walio majeruhi wanaweza wakatwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza.

Washika mitutu hao wa jiji la London waliwatandika Manchester City mabao 2-1 katika dimba la uwanja wa Emirates siku ya Jumatatu kwa ushindi huo sasa inamaanisha wameshinda michezo 11 kati ya 17 waliokwishacheza ya ligi hiyo.

Vijana hao wa Mzee Arsene Wenger's wameshinda michezo yote hiyo bila ya wachezaji wake hatari Jack Wilshere, Mikel Arteta, Santi Cazorla, Danny Welbeck, Tomas Rosicky na Francis Coquelin.

Mlinda mlango huyo Peter Cech anaamini baada ya kurejea kwa wachezaji wote hao waliomajeruhi wanaweza wakatwaa ubingwa wa ligi hiyo ifikapo mwezi May mwakani.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget