Meneja wa klabu ya Manchester City amesema Nahodha wa kjlabu hiyo Vicent Kompany anaweza kurejea dimbani akitokea kwenye majeruhi siku ya Boxing Day watakapokutana na klabu ya Sunderland.
Mlinzi huyo wa timu ya Taifa ya Ubelgiji alipata majanga hayo ya majeraha alipokuwa katika mchezo wao dhidi ya Aston Villa Novemba 8 mwaka huu ambapo mpaka mwisho wa mchezo huo uliisha kwa suluhu.
Kompany amekosa michezo mitano ya Ligi kuu soka nchini Uingereza dhidi ya klabu yake baada ya kupata majeraha hayo huku klabu yake ikipata ushindi katika michezo miwilina ikipoteza michezo mitatu ambapo wanatofautiana pointi 6 dhidi ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Leicester City katika msimamo wa Ligi hiyo.
City wamepoteza michezo mitano katika mzunguko huu wa kwanza katika ligi kuu soka nchini Uingereza lakini haijapoteza mchezo wakati Kompany akicheza.
Lakini Pellegrini anamatumaini makubwa ya mlinzi wake huyo mwenye umri wa miaka 29 kurejea na kuanza katika kikosi chake cha kwanza katika siku ya Boxing Day.
"Vincent anajitahidi kufanya mazoezi na wenzake na ninamatumaini siku ya jumamosi atakuwa sawa na kama Vincent akirejea katika kikosi cha kwanza ninaimani David na Sergio watacheza vizuri katika kila wiki na kujitahidi kufanya vizuri kila tunapokutana na wapinzani wetu”,Alisema Pellegrini.
Baada ya City kuwavaa Sunderland katika dimba la Etihad Stadium,watakuwa na michezo mingine mine ya nje ya dimba laokatika siku 12 ambapo watakutana na Leicester na Watford katika ligi, Everton katika Capital Cup huku klabu ya Norwich City wakikutana nayo katika kombe la FA Cup.
Post a Comment