Yakiwa yamesalia masaa machache kuwa
vaa Sunderland Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema anaamini
timu yake ndiyo yenye nguvu zaidi katika Ligi kuu soka nchini Uingereza
kutokana na kutokuwa na wachezaji wengi walio majeruhi.
City kwa sasa wanashika nafasi ya 3
katika ligi wakiwa na alama sita nyuma ya vinara Leicester baada ya kutandikwa
mabao 2-1 na Arsenal Jumatatu ya wiki hii.
Nahodha wao Vincent Kompany, 29, anatarajiwa
kurejea kikosini baada ya kukosa mechi tisa. Huku Mshambuliaji wao Sergio
Aguero naye amekosa michezo 11 kutokana na jeraha na akitarajiwa kurudi dimbani.
Ukiachana na wachezaji hao lakini
nae beki wao Pablo Zabaleta na kiungo wa kati Fernando pia wanatarajiwa kurejea
baada ya kuuguza majeraha yaliyokuwa yanawasumbua kwa muda mrefu.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.