Klabu ya soka ya Arsenal inadaiwa kuwa tayari kusikiliza ofa
kwa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil kama asipokubali kusaini
mkataba mpya.
Mkataba wa sasa wa nyota huyo mwenye umri wa miaka
28 unamalizika kiangazi mwaka 2018, lakini meneja wa Arsenal, Arsene Wenger
anaweza kumuuza kabla kama asipoongeza mkataba wake.
Wote wawili Alexis Sanchez na Ozil mikataba yao
inamalizika sawa na wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kuondoka Emirates.
Hata hivyo, Wenger anadaiwa kutotaka mkataba wa Ozil
uishe na anaweza kuamua kumuuza huku Chelsea, Manchester City na Juventus
zikidaiwa kumtaka.
Post a Comment