
KLABU ya Real Madrid imefikia rekodi ya kutofungwa
mechi 34 kufuatia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Borussia Dortmund katika michuano ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya jana.
Hata hivyo, matokeo hayo hayakutosha kuifanya Madrid
kufuzu hatua ya timu 16 bora wakiwa vinara wa kundi F baada ya kuzidiwa na
wapinzani wao Dortmund.
Madrid walionekana kumudu vyema mchezo kufuatia
mabao mawili mawili yaliyofungwa na Karim Benzema lakini mambo yalibadilika
baada ya mabao ya kusawazisha Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus.
Kipigo chao cha mwisho kilikuwa ni mabao 2-0
walichopata kutoka kwa Wolfsburg katika michuano hiyo Aprili 6 msimu uliopita
na toka wakati huo wamepata ushindi katika mechi 24 na kutoa sare tisa katika
mashindano yote huku wakifunga mabao 94 na kuungwa 31 pekee.
Post a Comment