
Hali ya mchezaji wa klabu ya soka ya Stand United Abdislim
Chidiebele inaendelea kutengemaa hivi sasa baada ya kutolewa kifaa maalumu
katika mdomo wake baada ya kuvunjika Taya.
Afisa habari wa klabu ya soka ya Stand united Deo
Makomba amesema kuwa mchezaji huyo anaendelea vyema hivi sasa na yupo mbioni
kuungana na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza.
Mbali na hilo makomba pia amezungumzia ratiba ya klabu
ya Stand United kwa sasa na kueleza kuwa wanatarajia kuwa na michezo ya
kirafiki kabla ya duru la pili la ligi kuanza.
Post a Comment