MSHAMBULIAJI wa Cristiano Ronaldo ameonyesha muonekano wake mpya wa nywere wakati akiwa katika mazoezi na klabu yake ya Real Madrid ikiwa ni kiashiria cha kusubiri sherehe za tuzo ya Ballon d'Or.
Mchezaji huyo raia wa nchini Ureno anauhakika kabisa wa kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya nne akiwa na muonekano mpya wa nywele.
Ronaldo ameiwezesha timu yake ya Taifa ya Ureno kutwaa taji la Euro 2016 nchini Ufaransa na kuiwezesha klabu yake ya Real Madrid kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani ulaya msimu uliopita.
Ronaldo anaonekana kuwa kivutio katika kuwania tuzo hizo akiwa pamoja na mchezaji mwenzake Lionel Messi na Antoine Griezmann kuwania tuzo hizo.
Ronaldo hatocheza katika mchezo wa kesho wakati timu yake ya Real Madrid itakapovaana na Deportivo la Coruna katika dimba la uwanja wa Santiago Bernabeu, huku kocha wake Zinedine Zidane akiwapa mapumziko wachezaji wake kadha kabla la kuanza kwa kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia nchini Japan.
Post a Comment