Klabu ya soka ya YANGA SC kesho inashuka dimbani kumenyana
na JKU ya Zanzibar katika dimba la Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo
wa kirafiki, ambao utakuwa wa kwanza tangu mabadiliko ya benchi la Ufundi mwezi
uliopita.
Novemba Yanga imeleta Maofisa wapya wawili wa benchi
la Ufundi, Kocha Mkuu George Lwandamina na Msaidizi, Noel Mwandila wote
Wazambia.
Siku hiyo mashabiki wa Yanga watapata fursa ya kumuona
kwa mara ya kwanza kiungo Mzambia, Justine Zulu aliyesajiliwa mapema mwezi huu.
Post a Comment