
Nyota wa klabu ya Real Madrid Pepe hupo huru hivi sasa kuanza mazungumzo na klabu yoyote baada ya kubakiza miezi 6 kabla ya mkataba yake kuisha.
Beki huyo wa kati wa timu ya Taifa ya Ureno mkataba wake unaisha June 30, 2017 kitu kinachomaanisha kuwa kuanzia January yupo huru kuanza mazungumzo na klabu yoyote huku ikionyesha wazi akivutiwa na soka la nchini Uingereza na kupata ofa nyingi kutoka China.
Pepe mwenye miaka 33 alikuwa ni moja ya wachezaji walioiwezesha nchi yake ya Ureno kutwaa taji la Euro 2016 na kuiwezesha klabu yake ya Madrid kushinda taji la Champions League msimu uliopita
Post a Comment