Inaripotiwa kuwa mcheza mpira wa
timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, na wachezaji wengine wa kandanda,
wamekwepa kodi ya mapato yao ya mamilioni ya dola, kwa kupitisha fedha hizo
kwenye njia za kuzighushi hadi nchi za n'gambo kusikotozwa kodi.
Habari hizo zimechapishwa na gazeti
moja la Ujerumani, Der Spiegel, na inasemekana zinatokana na data ya maelezo
pamoja na kandarasi, makubaliano ya siri na barua pepe.
Mawakili wa Ronaldo wanasema, wakuu
wa kodi wa Uspania wamekagua mapato yake na hawakuona kasoro yoyote.
Watu wengine maarufu wanaosemekana
kutajwa katika ufichuzi huo, ni pamoja na Jose Mourinho, meneja wa Manchester
United ambaye yeye na Ronaldo, anawakilishwa na wakala Jorge Mendes.
Post a Comment