Ligi ya vijana kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea katika vituo viwili vya Kagera na Dar Es Salaam ambapo duru la kwanza linatarajiwa kumalizika Desemba 05, 2016.
Katika kituo cha Dar es Salaam,
Simba ya Dar es Salaam inatarajiwa kucheza kesho Jumapili Novemba 4, 2016 na
JKT Ruvu ya Pwani katika mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana wakati saa 10.30
kutakuwa na mchezo kati ya Tanzania Prisons ya Mbeya na Ndanda FC ya Mtwara.
Kesho hiyo hiyo, Desemba 4, mwaka
huu katika kituo cha Kagera kutakuwa na mchezo kati Stand United ya Shinyanga
itakayocheza na Young Africans saa 8.00 mchana wakati ya Mwadui pia ya
Shinyanga itacheza na Mbao saa 10.30 jioni.
Jumatatu Desemba 5, mwaka huu ratiba
itakamilika katika kituo hicho cha Kagera kwa Kagera Sugar kucheza na African
Lyon ya Dar es Salaam saa 8.00 mchana wakati Azam FC ya Dar es Salaam na Toto
Africans ya Mwanza zitamaliza saa 10.30 jioni.
Kwa siku hiyo ya Jumatatu, Kituo cha
Dar es Salaam pia kutakuwa na mechi mbili ambako Majimaji ya Songea itacheza na
Ruvu Shooting ya Pwani saa 8.00 mchana wakati Mtibwa Sugar ya Morogoro itacheza
na Mbeya City ya Mbeya saa 10.30 jioni.
Hatua ya nusu fainali itachezwa jijini
Dar Es Salaam katika uwanja wa Azam Complex tarehe 09.12.2016 wakati fainali
itachezwa tarehe 11.12.2016 katika uwanja huo huo.
Post a Comment