
Mchezo wa
kirafiki uliokuwa ufanyike hii leo kati ya Mbao FC na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza umehairishwa kutokana na kuingiliana
kwa matumizi ya uwanja.
MALINZI amesema kuwa mchezo huo ulikuwa maalumu kwa ajili ya kutoa heshima kwa marehemu Ismail Khalfan - mchezaji wa timu ya vijana ya Mbao aliyefariki dunia Desemba 4, mwaka huu wakati akiiitumikia timu yake ya vijana kwenye mchezo wa Ligi ya Vijana ya TFF U20 dhidi ya Mwadui, uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Kadhalika, mchezo huo utatumika kama kuzipima nguvu timu hizo baada ya mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) hivyo wadau wote wa michezo wameombwa kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuchagia rambirambi ya familia hiyo ambayo kwa pamoja na wanafamilia ya soka walipoteza hazina nyingine muhimu kwenye mpira wa miguu
Post a Comment