Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umebainisha
mipango yake ya kuanza ujenzi wa uwanja wao uliopo maeneo ya Bunju mapema mwezi
January mwakani ili uweze kutumika na wachezaji wa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa klabu
hiyo Haji Manara amesema kwa sasa wapo katika hatua nzuri ya kuhakikisha
January mwakani uwanja huo unaanza kujengwa ili uweze kutumia na wachezaji wa
klabu hiyo ambapo kwa hivi sasa wanatumia fedha nyingi kwajili ya kukodi
uwanja.
Manara amesema kwa sasa klabu hiyo imeanza hatua
kadhaa za kuhakikisha kufikia mwakani wanaanza ujenzi huo hivyo kwa sasa
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zacharia Hans poppe ameanza
kushughulika ujenzi huo ambao unatarajiwa kuleta mapinduzi ya kisoka kwa upande
wao.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.