Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Liverpool Jurgen
Klopp amesema alikuwa wa kwanza kufatwa kwaajili ya kuifundisha klabu ya Manchester
United's lakini aligoma kuiacha klabu yake ya Borussia Dortmund.
Klopp amesema yeye ndiye alikuwa chaguo la kwanza kuwanoa
Mashetani wekundu hao baada ya aliyekuwa kocha wao Alex Ferguson kuiacha klabu
hiyo lakini yeye mwenyewe aligoma kuiacha klabu yake ya Dortmund.
Kocha huyo mwenye miaka 48 alianza kuifundisha
klabu ya Liverpool kwa mara ya kwanza baaada ya kuchukua mikoba ya Brendan Rodgers
mwezi October mwaka jana.
Klopp amesema alipata ofa nyingi za kuondoka nchini Germany
lakini mwenyewe alikua anahitaji kuendelea kubaki katika klabu yake ya Dortmund,
na katika ofa hizo klabu ya United ilikuwa klabu ya kwanza kumuhitaji mwezi April
mwaka 2013 baada ya kocha wao Sir Alex Ferguson kubwaga manyanga.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.