Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Liverpool
Jurgen Klopp amelalamikia mfululizo wa mechi Ligi kuu nchini Uingereza wakati
wa sikukuu za Krismasi hadi kuingia Mwaka Mpya kuwa kunakiporomosha kiwango cha
soka nchini England kufanya vizuri katika mashindano makubwa.
Mjerumani huyo amekiri kuwa
Wachezaji wa England wana vipaji vikubwa lakini kwa kukosa kwa kukosa kwao
mapumziko ya wakati huu wa Majira ya Baridi kutaiathiri England Mwezi Juni
kwenye Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, zitakazochezwa Nchini Ufaransa.
Klopp ameeleza, kuwa England chini
ya kocha wake Roy Hodgson, wanapaswa kutwaa EURO 2016 kwa vile wana vipaji
vikubwa.
Klopp pia amesema hivi sasa Ligi
zote kubwa Ulaya, La Liga ya Spain, Bundesliga ya Germany na Serie A ya Italy,
pamoja na nyingine kadhaa,hazina mapumziko ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka
Mpya.
Siku ya kesho Jumamosi Liverpool watakuwa
na kibarua kizito watakapokuwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Anfield kuwavaa
Vinara wa Ligi Leicester City.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.